.: VYUO NILIVYOOMBA KWA PhD 2015                                                          

VYUO NILIVYOOMBA KWA PhD 2015

    
Unapotaka kuomba udhamini wa elimu ya juu, fahamu kuwa mwombaji hauko peke yako. Kuna maelfu ya watu kila siku wanatafuta udhamini tena kwa fani kama hiyohiyo unayotaka kusoma. Idadi ya vyuo unayoomba na unaombaje ni vitu muhimu sana. 

Huu ni mtazamo wangu: Christiano Ronaldo, Messi (kwenye soka), Kobe, Lebron nk (Basketball) sio wachezaji wa ajabu sana kwa kuangalia uwezo wao wa kufunga magoli. It's Math. If you make so many shots on target, you are going to score. If you don't shoot towards the goal, you don't score. As simple as that. Hichi ndicho Ronaldo, Messi, Neymar, Bale nk wanachokifanya. Wanahakikisha wanapiga mashuti mengi golini ili wafunge. Ukiangalia Balotelli, Torres na Adebayor wamejitahidi kupiga mashuti, ila mashuti yao mengi hayakulenga goli, na yale yaliyolenga goli hayakuwa na nguvu ya kutosha, na mengine yalikutana na kipa makini kuyazuia.

Kutokana na kuamini, mashuti mengi golini, upigaji kwa ufundi wa mashuti hayo, kumuangalia kipa yupo wapi wakati unapiga mashuti hayo inakufanya upate idadi kubwa ya magoli ya kushinda. Hivyo kwangu nimeangalia mambo mengi ninapoomba vyuo. 

Vitu nilivyoangalia ninapoomba vyuo ni vifuatavyo:Baada ya kuangalia vitu hivi, kinachofuata sasa ni kupiga mashuti golini. Nimeshajua golikipa amekaaje, walinzi wapoje na nipigeje. Nilichofanya ni kupiga mashuti mazito golini. Nimeweza kuomba vyuo 16 hadi sasa nikiamini kuwa ni lazima nipate chuo walau kimoja. Itakuwa ngumu mno kupiga mashuti 16 golini kisha nikose goli hata moja. Maana namepitia kila nyanja kuangalia nipigeje na nimepiga vyema.

Vyuo nilivyoomba, mahali vilipo na programs ni kama ifuatavyo

PhD PROGRAMS
1.      University of Georgia at Athens (GEORGIA) – PhD in Political Science and International Affairs
2.      University of Georgia at Athens (GEORGIA) – PhD in Public Administration and Public Policy
3.      Tennessee State University (TENNESSEE) – PhD in Public Administration
4.      Universality of Missouri (MISSOURI) – PhD in Political Science
5.      Washington University in St. Louis (MISSOURI) – PhD in Political Science
6.      West Virginia University (WEST VIRGINIA) – PhD in Political Science
7.      George Mason University (VIRGINIA) PhD in Conflict Analysis and Resolution
8.      Kennesaw State University (GEORGIA) – PhD in International Conflict Management
9.      University of Texas at Austin (TEXAS) PhD in Government
1.   Arizona State University (ARIZONA) – PhD in Justice Studies
1.    University of Michigan (MICHIGAN) – PhD in Political Science
1.    Western Michigan University (MICHIGAN) – PhD in Political Science
1.    Kent State University (OHIO) – PhD in Political Science (Conflict Resolution concentration)
1.    University of South Dakota (SOUTH DAKOTA) – PhD in Political Science
1.   University of Hawaii at Manoa (HAWAII) – PhD in Political Science
1.   Florida International University (FLORIDA) –PhD in Political Science


MUHIMU:
Makala hii sio ya kujadili soka ya nani ni bora au timu gani inafanya vizuri. Ninatumia baadhi ya wachezaji, na baadhi ya timu kwa kujaribu kueleza kwa mifano dhahiri na kuweka vitu katika perspective. 

MAKULILO

ernest_makulilo@yahoo.com